Mtoto Mussa apotea kwa mazingira tatanishi

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:02 PM Apr 16 2025
 Mussa Suleiman
Picha: Nipashe Digittal
Mussa Suleiman

MWANAFUNZI wa darasa la tatu katika shule ya msingi Salasala, Dar es Salaam, Mussa Suleiman (8), amepotea katika mazingira ya kutatanisha, baada ya kutumwa dukani.

Akizungumzia na Nipashe Digital kuhusu tukio hilo, Hamisa Haruna, ambaye ni mama mzazi wa mtoto huyo, amesema ametoweka Machi 14, 2025, baada ya kutumwa dukani lakini hakurejea tena nyumbani.

“Tumemtafuta hadi leo hatujafanikiwa kumpata, tumetoa taarifa polisi,” amesema mama huyo.

Amesema kabla ya kutoweka mtoto huyo alikuwa amevaa bukta jezi ya Simba na fulana ya kijani, RB namba SAL/RB471/2025 atakayefanikiwa kumuona awasiliane na mzazi kwa namba 0767952636 au apelekwe kituo cha polisi chochote.