Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust, ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Mbeya Mjini, Dk. Tulia Ackson, leo ameongoza mamia ya wananchi wa Mkoa wa Mbeya katika zoezi la upimaji macho na utoaji wa matibabu bure.
Zoezi hilo ambalo linatolewa kwa siku tatu mfululizo, limeanza rasmi katika Shule ya Msingi Kagera, iliyopo Kata ya Ilomba, na linatolewa kupitia ushirikiano kati ya Tulia Trust na The Bilal Muslim Mission of Tanzania.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Dk. Tulia amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na huduma hizo muhimu, akibainisha kuwa afya bora ni msingi wa maendeleo ya mtu binafsi na jamii kwa ujumla.
"Taasisi ya Tulia Trust itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo kutoa huduma mbalimbali zenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi. Afya ya macho ni eneo ambalo wengi hulipuuza, lakini lina athari kubwa kwa maisha na ustawi wa kila siku," amesema Dk. Tulia.
Huduma zinazotolewa katika zoezi hilo ni pamoja na:
Wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo wameeleza kufurahishwa na hatua hiyo ya kuwafikia moja kwa moja katika maeneo yao, wakisisitiza kuwa huduma hiyo imeleta unafuu mkubwa kwa familia nyingi ambazo haziwezi kumudu gharama za upimaji wa macho.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED