Tundu Lissu yupo gereza la Ukonga

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 01:44 PM Apr 19 2025
Tundu Lissu
PICHA: MTANDAO
Tundu Lissu

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),kimesema kuwa kimekutana na uongozi wa Jeshi la Magereza na kujulishwa kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho,Tundu Lissu amehamishiwa Gereza la Ukonga.

Taarifa kwa umma iliyotolewa leo Aprili 19,2025 na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA,Brenda Rupia imeeleza kuwa viongozi wakuu wa chama wamekutana na uongozi wa Jeshi la Magereza na kufahamishwa mabadiliko hayo.
"Kufuatia taarifa hiyo, familia, wanachama wa CHADEMA na Watanzania wote waliokuwa na wasiwasi kuhusu mahali alipo Lissu kuwa sasa wanaweza kumtembelea kwa kufuata taratibu za kawaida za kumuona mahabusu katika Gereza hilo,"amesema.
Brenda amesema Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara, John Heche, anatarajiwa kufika Gereza la Ukonga leo Aprili 19,2025 kwa ajili ya kumwona Lissu na kuzungumza naye kuhusu hali yake.