Watu saba wamefariki dunia, huku wengine 15 wakijeruhiwa baada ya ajali kutokea ikihusisha gari la kubeba wagonjwa (ambulance) na toyo huko Luganga, Mafinga mkoani Iringa.
Akizungumza kutokea eneo la ajali alipokuwa akitembelea majeruhi, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Dk Linda Salekwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akisema taarifa zinaonesha watu waliokuwa katika toyo hiyo walikuwa wanakwenda shambani.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED