Waandishi wa Habari mkoani Shinyanga,wametembelea bustani ya wanyama “Jambo Zoo”iliyopo maeneo ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga ambayo inamilikiwa na Kampuni ya Jambo Group.
Ziara hiyo imefanyika leo Aprili 19,2025 ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani, pamoja na kuwaunga mkono wawekezaji wazawa,ziara ambayo imeratibiwa na Klabu ya waandishi wa habari mkoani humo.
Mhifadhi wa Jambo Zoo Babuu Burhan Kajuna,akizungumza na waandishi wa habari,amesema wana wanyama wa aina mbalimbali ambao wamepewa mafunzo pamoja na kuwazoea binadamu na hata kupiga nao picha kwa ukaribu kabisa na kuwalisha chakula.
“Tunawashukuru waandishi wa habari kwa kutembelea Jambo Zoo,pia tunawakabirisha wananchi wa wote waje wafanye utalii wa ndani hapa Shinyanga, na bei zetu ni rafiki kabisa,”amesema Kajuna.
“Ukifika hapa Jambo Zoo utajifunza mambo mbalimbali kuhusu Wanyama na tabia zao,pamoja na kupiga nao picha kwa ukaribu kabisa na kuwalisha chakula kwa mkono wako,”ameongeza.
Mratibu wa “Tour hiyo”Marco Maduhu, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Tendaji Klabu ya waandishi wa habari na mfadhili wa safari hiyo,ameipongeza Kampuni ya Jambo kwa uwekazaji wa Bustani hiyo ya Wanyama, na kumuunga Mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhamasisha utalii wa ndani kupitia Filamu ya The Royal Tour.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED