Kanuni: Marufuku simu kituo cha kupiga kura

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:03 PM Apr 18 2025
Kanuni: Marufuku simu  kituo cha kupiga kura
Picha: Mtandao
Kanuni: Marufuku simu kituo cha kupiga kura

Kanuni za maadili ya uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani za Mwana 2025 zimeweka marufuku kwa mtu yeyote kutumia simu ya kiganjani au kifaa kingine cha mawasiliano ndani ya kituo cha kupigia, kuhesabia au kujumlishia kura.

Aidha,wanaoruhusiwa kuwa na vifaa hivyo ni msimamizi wa uchaguzi, msimamizi msaidizi wa uchaguzi, msimamizi wa kituo, wasaidizi wake na mlinzi wa kituo cha kupigia kura ambao watatumia simu zao au kifaa kingine cha mawasiliano pale itakapobidi kwa shughuli za uchaguzi tu.

Pia kwa walioruhusiwa wanatakiwa kuondoa mlio na kuwa kwenye mtetemo kwenye simu zao au vifaa.

Aidha, kiongozi, mgombea au mtendaji wa chama cha siasa, mwanachama au mfuasi kujihusisha na kuwahamasisha wanachama au wafuasi kupiga kura zaidi ya mara moja katika uchaguzi mmoja.

Vile vile, kununua kadi ya mpiga kura, kukusanya kadi za wapiga kura au kuharibu kura; kutoa hongo, zawadi, kununua kura, shukrani au aina yoyote ya malipo ya fedha au vifaa kwa mpiga kura au mtendaji wa uchaguzi.