Wasira uso kwa uso na Kadinali Rugambwa

By Maulid Mmbaga , Nipashe
Published at 06:18 PM Apr 16 2025

Makamu Mwenyekiti wa CCM Stephen Wasira akizungumza na Kadinali Protase Rugambwa, leo Tabora.
Picha Maulid Mmbaga.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Stephen Wasira akizungumza na Kadinali Protase Rugambwa, leo Tabora.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amekutana na kufanya mazungumzo na Muadhama Kadinali Protase Rugambwa katika Jimbo Kuu Katoliki la Tabora.

Wasira amekutana na Kadinali Rugambwa leo Aprili 16, 2025 katika Jimbo Kuu Katoliki Tabora akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 mkoani Tabora.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejadili mambo mbalimbali kuhusu umuhimu wa kudumisha amani na ustawi wa jamii na Tanzania kwa ujumla.

Aidha baada ya mazungumzo hayo Wasira amefanikiwa kutembelea Shule ya Sekondari  St. Mary's ambayo imebeba historia kubwa kama shule ya kwanza ambayo Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alifundisha kwa miaka mitatu.