Mbunge ataka wakalimani lugha ya alama uchaguzi mkuu 2025

By Paul Mabeja , Nipashe
Published at 03:06 PM Apr 14 2025
Mbunge wa Viti Maalum, Stella Ikupa.
Picha: Mtandao
Mbunge wa Viti Maalum, Stella Ikupa.

Mbunge wa Viti Maalum, Stella Ikupa, bungeni, imesema serikali inapaswa kuweka wakalimani wa lugha ya alama kwenye mikutano ya kampeni wakati wa uchaguzi mkuu mkuu 2025, ili kuwezesha makundi ya watu wenye ulemavu hususani viziwi kupata fursa ya kusikia sera za wagombea mbalimbali.

Ikupa, amesema hayo leo Aprili 14, bungeni jijini Dodoma wakati akichangia mjadala wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu katika mwaka wa fedha 2025/2026.

Amesema viziwi ni wapigaji wa kura wazuri lakini hawezi kufanya hivyo bila kupata wakalimani wa lugha za alama ambao watawasaidia kujua sera za wagombea katika mikutani mbalimbali ya kampeni.

“Mweshimi Mwenyekiti mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi naomba niishauri serikali yangu sikivu kutoa maelekezo na kusisitiza matumizi ya wakarimani wa lugha ya alama katika uchaguzi mkuu mwaka huu ili hawa wenzetu waweze kushiriki kuchagua wagombea watakao wataka baada ya kusikia sera zao,”amesema