Rais Samia atoa salamu za pole kifo cha Sheikh Hassan Daher

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 08:05 PM Apr 14 2025
Rais Samia atoa salamu za pole kifo cha Sheikh Hassan Daher
Picha: Mtandao
Rais Samia atoa salamu za pole kifo cha Sheikh Hassan Daher

Rais Samia Suluhu Hassan, amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Sheikh Hassan Daher, Sheikh wa Wilaya ya Igunga, Mkoa wa Tabora.

Katika taarifa yake katika Channel yake ya WhatsAaap, Rais Samia amesema Sheikh Hassan alikuwa ni kiongozi wa dini aliyeheshimika, mwalimu wa wengi katika imani, na mtu aliyesimamia misingi ya upendo, umoja, amani na utulivu wa nchi yetu. Alijitolea kufundisha na kuhimiza maadili mema, akiacha alama kubwa ya uongozi wa kiroho katika jamii.

Rais Samia ametuma salamu za pole kwa familia ya marehemu, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dk. Abubakar Zubeir Ali Mbwana, Waislamu wote, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

"Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un"