Askofu Shoo: Polisi msikubali kutumiwa kwa maslahi ya watu

By Godfrey Mushi , Nipashe
Published at 10:56 AM Apr 20 2025
Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Frederick Shoo,
Picha: Mtandao
Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Frederick Shoo,

ASKOFU wa Dayosisi ya Kaskazini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Frederick Shoo, ameliomba Jeshi la Polisi nchini, katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa Rais, Wabunge na Madiwani, wasikubali kutumiwa kwa maslahi ya watu ambao hawaitakii mema nchi.

"Jeshi letu la Polisi, nawaombeni kweli, Polisi tunawaombeni sana. Tunawategemea sana katika jambo la ulinzi na usalama na wote wanaohusika.

Zaidi aliongeza, "Niwaombe katika uchaguzi huu. Kila mmoja kwa dhamiri yake aangalie hilo na usikubali utumiwe kwa maslahi ya watu ambao hawaitakii nchi hii mema. Polisi nawaomba msisahau wajibu wenu na Mungu awasaidie."