Watanzania waaswa kulinda amani ya taifa

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 11:52 AM Apr 20 2025
Askofu wa Jimbo Katoliki Ifakara, Mhashamu Salutaris Libena
Picha: Mtandao
Askofu wa Jimbo Katoliki Ifakara, Mhashamu Salutaris Libena

ASKOFU wa Jimbo Katoliki Ifakara, Mhashamu Sulutaris Libana, amewataka watanzania kudumisha amani na kuzingatia makubaliano na maelewano, kwa kuwa ndiyo msingi wa amani.

"Sisi kama nchi tunafurahia amani, tunasema tuna amani na ni kweli, tuna amani kwani hatuna vita hatuna magomvi, amani iendane na upendo, iwe zao la ukweli na amani inatokana na upendo, amani inahitaji sana makubaliano na maelewano," amesema Askofu Libana.

Askofu Libana ameyasema hayo leo, Aprili 20, 2025, alipokuwa akitoa mahubiri wakati wa ibada ya Pasaka kitaifa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Andrea Mtume, Jimbo Katoliki lililopo Ifakara, mkoani Morogoro.