Prof. Muhongo ataka maboresho sera ya Maafa

By Paul Mabeja , Nipashe
Published at 04:55 PM Apr 14 2025
Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhungo.
Picha:Mtandao
Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhungo.

Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), ProfeSa Sospeter Muhungo, amesema Sera ya Taifa ya Maafa inahitaji marekebisho makubwa ili iendane ha halihalisi iliyopo hivi sasa.

Prof. Muhongo, amesema hayo leo Aprili 14, bungeni jijini Dodoma, wakati akichangia mjadala wa bateji ya Ofisi ya Waziri Mkuu katika mwaka wa fedha 2025/2026.

“Sera yetu tuliyonayo hivi sasa haiendani na halihalisi kwasababu maafa yamekuwa ni mengi na ya aina tofautitofauti kwa mfano sasa tunamaafa yanayotokana na mabadiliko tabianchi hayo ni kama ukame, mafuriko, dhoruba huko ziwani na mengine.

Amesema sababu ya pili ya kufanyika kwa maboresho ya sera hiyo ni ongezeko la idadi ya watu lililopo hivi sasa.

“Kutokana na hali hiyo maafa yakitokea sera haiendani na hali halisi ya kukabiliana nayo, mwaka 1961 wakati nchi yetu inapata Uhuru tulikuwa watu karibu milioni 10 sasa hivi mwaka huu tukifika mwisho tutakuwa tumevuka milioni 70,”amesema