Nyayo watoto wachanga kutumika usajili NIDA

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 05:08 PM Apr 14 2025
Nyayo za mtoto
Picha: Mtandao
Nyayo za mtoto

MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imesema itaanza kusajili watoto wachanga kuanzia umri sifuri, kwa kutumia alama za nyayo zao.

Amesema hatua hiyo ni mpango serikali katika kuziunganisha huduma za kijamii na mfumo wa mamlaka hiyo na taasisi za umma hasa kwa mahitaji ya kupata nakala muhimu ikiwamo Pasi ya kusafiria.

Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji (Picha: Christina Mwakangale)
Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo, Aprili 14, 2025.

Amesema mpango huo malengo yake ni kusajili nchi nzima watoto wa umri huo hadi kwa wenye umri chini ya miaka 18.