KATIKA dunia ya sasa inayotawaliwa na teknolojia, uwekezaji katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), si hiari, bali ni hitaji la msingi kwa maendeleo ya taifa.
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais–TAMISEMI, imewajengea uwezo walimu ili watumie TEHAMA kama daraja la kufundisha maarifa ya kisasa, shule za msingi hadi taasisi za elimu ya juu, lakini kwanza msingi na sekondari.
Kupitia mradi wa Kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP), walimu wa sekondari wanapatiwa mafunzo ya kutumia TEHAMA, ikiwamo vifaa kama vishikwambi, maabara za kompyuta na mifumo ya kidijitali kama Learning Management System (LMS), anasema Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Franklin Rwezimula, anasema katika awamu ya hivi karibuni, walimu 2,632 kutoka mikoa 17 wanashiriki mafunzo hayo katika vyuo vya ualimu Monduli mkoa wa Arusha na Butimba mkoa wa Mwanza.
Hata hivyo, anatoa wito kwa wanawake, akisema ni wachache, asilimia saba pekee ndiyo wameshiriki, anaongeza Naibu Katibu Mkuu.
Anaeleza kuwa kupitia mafunzo hayo, walimu hujifunza kuandaa masomo kwa kutumia programu za kompyuta kama word, excel, powerpoint na multimedia, pamoja na kupata ujuzi wa kutafuta vitabu mtandaoni na kufanya matengenezo madogo ya kompyuta zaidi ya hayo, walimu wamepewa jukumu la kusambaza maarifa hayo kwa wenzao mashuleni ili TEHAMA iwe sehemu ya utamaduni wa ufundishaji.
Akizungumza wakati wa uzin duzi wa mafunzo hayo, Naibu Katibu Mkuu, Dk. Rwezimula, anasema serikali inataka kila mwanafunzi apate maarifa sahihi kulingana na mahitaji ya karne ya 21 vilevile walimu waliopata mafunzo hayo wanapaswa kuwa mabalozi wa mabadiliko.
Anaongeza kuwa kupitia Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 (toleo la 2023), serikali imeweka mkazo kwenye TEHAMA kuanzia shule za msingi hadi sekondari.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, anasema katika karne hii ya kidijitali, taifa haliwezi kuendelea kutegemea mbinu za zamani kufundisha watoto, na kwamba TEHAMA ni njia ya kisasa inayorahisisha, kuboresha na kupanua upatikanaji wa maarifa.
Anasisitiza kuwa TEHAMA ni kichocheo cha uchumi wa viwanda kwa kuwaandaa vijana kuwa wabunifu, wajuzi na wenye fikra za kimapinduzi.
VIPI WANAWAKE?
Changamoto ya ushiriki mdogo wa walimu wanawake katika mafunzo hayo imeibua wito wa kuongeza mazingira rafiki na ya motisha ili kuhimiza usawa wa kijinsia katika TEHAMA. “Walimu wanawake wana nafasi muhimu ya kuwahamasisha wanafunzi wa kike kuvutiwa na TEHAMA, na hivyo kupunguza pengo la kijinsia kwenye sekta ya teknolojia , ” a n a s e m a Prof. Mkenda.
Anaongeza kuwa wizara hiyo imeanza k a m p e n i maalum za kuhamasisha wanafunzi wa kike kushiriki masomo ya sayansi na teknolojia, sambamba na kuanzisha mkondo wa amali kwa wanafunzi wenye vipaji vya kiufundi. Kwa mujibu wa Jarida la Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwaka 2021, kuenea kwa TEHAMA kumeambatana zaidi na matumizi ya Kiingereza na lugha nyingine za kigeni huku Kiswahili kikiwa nyuma.
Tafiti nyingine mathalani, Umuhimu na changamoto za TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kwa wageni, zinaonyesha teknolojia imesaidia walimu na wanafunzi kujifunza lugha za kigeni, lakini kuna pengo kubwa katika matumizi ya TEHAMA kufundishia Kiswahili, hasa kwa wageni.
Mwalimu Neema Joseph wa Sekondari ya Ilemela, Mwanza, anasema alikuwa na hofu kutumia kompyuta darasani, lakini sasa anaweza kuandaa somo lote kwenye kishkwambia ‘tablet’ na kufundisha bila kutumia ubao hivyo imerahisisha ufundishaji.
N e e m a a n a t a j a changamoto kama uhaba wa vifaa, mtandao wa intaneti unaoyumbayumba na nakala zisizo sahihi mtandaoni. Kaimu Ofisa Elimu Mkoa wa Mwanza Justina Mombeki anasema dhamira ya serikali ni kuboresha sekta ya elimu kwa kujenga shule mpya na miundombinu kwa wanafunzi wote wanaofaulu kupata nafasi za kusoma.
Anaeleza kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imepewa dhamana ya kumuandaa Mtanzania aliyeelimika, mwenye maarifa, stadi, umahiri, uwezo na mtazamo chanya ili achangie katika maendeleo ya taifa.
Anaongeza kuwa mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanahama kutoka katika matumizi ya karatasi na kuingia kwenya anga la dijitali kurahisisha utendaji kazi, aidha, anawasihi washiriki kuacha kutanguliza maslahi binafsi bali ya umma kwa kufanya kazi ambazo zitasaidia watu wengi kunufaika mfano kuwapa ujuzi wa TEHAMA walimu wengine ambao hawajapata mafunzo hayo.
Anawasisitiza walimu kuwa wabunifu na kuacha kufanya mambo kwa mazoea hali inayoshusha ufanisi wa utendaji kazi na kwamba ubunifu uta wasaidia kuwa washindani katika kupata matokeo chanya yanayolenga kumpa mwanafunzi ujuzi na maarifa.
Anawataka kuwa mabolozi wazuri wa kueleza juhudi zinazofanywa na serikali katika kuboresha sekta ya elimu na kuinua uchumi wa Taifa kwa ujumla.
Ili kuimarisha matumizi ya TEHAMA kwenye shule za sekondari, wadau wanashauri, ziandaliwe semina za mara kwa mara kwa walimu, kuhakiki sha vifaa vinapatikana kwa wingi na ubora, kuongeza uwekezaji kwenye taasisi binafsi na za umma na kuweka mkazo katika mitaala, hasa kwa lugha kikiwamo Kiingereza na Kiswahili na nyingine za kigeni
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED