15 wakamatwa kwa kuharibu tangazo la Museveni

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:51 PM Jul 15 2025
news
Picha Mtandao
Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Wanachama 15 wa chama cha upinzani cha National Unity Platform nchini Uganda, wameshtakiwa kwa kuharibu mabango ya kampeni ya Rais Yoweri Museveni, jambo lililochukuliwa kama ni kinyume na sheria.

Ilielezwa kuwa tukio hilo lilitokea leo, huku Polisi wakisema 15 hao waliharibu mabango katika mji mkuu wa Kampala siku chache kabla ya ziara ya Rais Museveni katika eneo hilo.

“Washukiwa wanashtakiwa chini ya Kifungu cha 78 (2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Urais, ambayo inaharamisha upotoshaji wa matangazo na nyenzo za kampeni,” ripotia ya tuvuti aya Chimp amesema.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa washukiwa hao wanazuiliwa katika gereza la Luzira na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani Julai 29, mwaka huu.

Kukamatwa kwa watu hao kunakuja huku joto la kisiasa likipanda baada ya Museveni kuteuliwa Julai tato, mwaka huu kama mgombea wa chama tawala cha National Resistance Movement katika uchaguzi wa rais wa Januari ujao.

Vile vile, imeelezwa kuwa iwapo atachaguliwa tena, Museveni mwenye umri wa miaka 80, ambaye aliingia madarakani mwaka 1986, anaweza kuendeleza utawala wake hadi takriban miaka 50.