Lamine Yamal matatani kuwaajiri wenye ualibino kutumbuiza

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:25 PM Jul 15 2025
news
Picha Mtandao
Winga wa Barcelona Lamine Yamal.

Wizara ya Haki za Kijamii ya Uhispania imeitaka ofisi ya mwendesha mashtaka wa nchi hiyo kumchunguza winga wa Barcelona Lamine Yamal baada ya kuripotiwa kuwaajiri watu wenye ulemavu wa ngozi ili kutumbuiza kwenye sherehe yake ya kutimiza miaka 18.

Yamal aliandaa sherehe hiyo Jumapili katika nyumba iliyokodishwa huko Olivella, mji mdogo ulio kilomita 50 kaskazini magharibi mwa Barcelona, na wageni wakiwemo WanaYouTube, washawishi, na wachezaji wenzake kadhaa wa Barcelona.

Inadaiwa Yamal alikodisha kikundi cha watumbuizaji walio na unyonge, jambo ambalo Chama cha Watu wenye ‘Achondroplasia’ na ‘Dysplasias’ nyingine za Mifupa nchini Uhispania (ADEE) kilieleza kuwa halikubaliki katika karne ya 21.

“ADEE imewasilisha malalamiko, kwa hivyo wizara hii imeitaka ofisi ya mwendesha mashtaka kufanya uchunguzi ili kuona ikiwa sheria imekiukwa, haki za watu wenye ulemavu zizingatiwe,” Wizara ya Haki za Kijamii ya Uhispania iliambia shirika la habari la AFP.

ADEE ilisema inashutumu hadharani uajiri wa watu wenye ulemavu wa ngozi kama sehemu ya burudani, na itachukua hatua za kisheria kwakuwa inaendeleza dhana potofu, inachochea ubaguzi, na inadhoofisha taswira na haki za watu hao.

Katika taarifa ilisema: “Vitendo hivi vinakiuka sio tu sheria za sasa lakini pia maadili ya kimsingi ya jamii inayotaka kuwa na usawa na heshima.

“Sheria ya jumla juu ya haki za watu wenye ulemavu inakataza kwa uwazi vitendo vifuatavyo: Maonyesho au shughuli za burudani ambazo watu wenye ulemavu au hali zingine hutumiwa kuchochea dhihaka, au kejeli kutoka kwa umma kwa njia inayopingana na heshima inayostahili utu ni marufuku,” ilisema sehemu ya taarifa.

Hata hivyo, kituo cha redio cha Uhispania RAC1, external kilitangaza mahojiano na mtu aliyedai kuwa mmoja wa waburudishaji waliokuwepo kwenye tafrija hiyo ambaye alimtetea Lamine Yamal.

“Hakuna aliyetudharau, tulifanya kazi kwa amani. Sielewi kwa nini kuna hype nyingi. Sisi ni watu wa kawaida, ambao hufanya tunachotaka, kwa njia ya kisheria kabisa.
“Tunafanya kazi kama watumbuizaji. Kwa nini hatuwezi kufanya hivyo? Kwa sababu ya hali yetu ya kimwili? Tunajua kikomo chetu ni nini na hatutawahi kuvuka: sisi sio nyani wa ardhini,” alisema msanii huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina.

Mwigizaji huyo alisema ilichukua saa moja, na baadaye watumbuizaji wakajiunga na tafrija hiyo. “Tunacheza, tunasambaza vinywaji, tunafanya uchawi ... kuna aina nyingi za maonyesho. Kila mtu alikuwa na wakati mzuri.”

Alipotafutwa kwa maoni na BBC Sport, msemaji wa Barcelona alisema klabu hiyo “Haikuwa katika nafasi ya kutoa maoni juu ya kitendo ambacho kiko ndani ya nyanja ya kibinafsi”.