TCU yafungua dirisha la udahili

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 10:54 AM Jul 15 2025
Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa, ametangaza kufunguliwa kwa dirisha la udahili kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza katika Taasisi ya Elimu ya Juu nchini kwa mwaka wa masomo 2025/26.

Ameyasema hayo leo Julai 15, 2025, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ambapo amesema dirisha hilo litakuwa wazi hadi Agosti 10, 2025.

"Tume inawaasa wananchi kuepuka kutapeliwa na watu wanaojiita mawakala au washauri wanaodai wanatoa huduma ya namna ya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu hapa nchini,"amesema.


Amesema maombi ya udahili wa kujiunga na Shahada ya Kwanza yanahusu makundi matatu,  wenye sifa stahiki za Kidato cha Sita, Shashahada (diploma) au sifa linganifu na wenye sifa stahiki za Cheti  cha Awali cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Amesema maombi yatumwe moja kwa moja kwenye vyuo ambavyo mwombaji amevichagua na kuchagua program za masomo anazozipenda.

"Maelekezo mahususi ya namna ya kutuma maombi yanatolewa na vyuo husika," amesema Prof. Kihampa.