CCM yaomba kura CHADEMA

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 06:05 PM Apr 12 2025
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA  Amos Makalla
PICHA: MTANDAO
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makalla

Baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoshiriki kusaini makubaliano ya kanuni za uchaguzi, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimewaomba wanachama wa chama hicho kwa kuwa walijiandikisha, wakati wa upigaji kura wakakichague CCM.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA  Amos Makalla, aliyasema hayo leo wilayani Nachingwea, mkoani Lindi, katika mkutano wa hadhara, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya siku 10 katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Anasema leo ilikuwa tarehe ya mwisho ya vyama vya siasa kusaini makubaliano hayo , lakini vyama vyote vimeshiriki kusaini maana yake ndivyo vitashiriki uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
“Kwa bahati mbaya lakini si bahati mbaya wale waliokuja hapa wameamua mwaka huu wapumzike wamechoka sana. 
“Hawa hawajajiandaa na uchaguzi wana migogoro hawajaenda kusaini maana yake hawatashiriki uchaguzi huu.
“Kama kuna mwana CHADEMA hapa na si ni haki ya mtu kupigakura, CHADEMA  haipo, uchaguzi ukifika pigia CCM.