Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Gissima Nyamo-Hanga, unatarajiwa kuzikwa Jumatano, Aprili 16, 2025, nyumbani kwao Mingungani, Bunda mkoani Mara.
Nyamo-Hanga na dereva wake walifariki dunia usiku wa kuamkia Jumapili baada ya ajali ya gari kutokea wilayani Bunda. Polisi wamesema ajali ilisababishwa na dereva wa gari walilokuwamo kumkwepa mwendesha baiskeli na kugongana na lori.
TANESCO imetangaza kuwa maombolezo yatafanyika leo na kesho nyumbani kwa marehemu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Nyamo-Hanga aliteuliwa na Rais Samia Septemba 2023 kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, akitokea REA.Baada ya kuteuliwa alikabiliana na changamoto za umeme nchini na alifanikiwa kuzitatua kwa kiasi kikubwa.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED