Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kati, Jackson Jingu, ameibua hoja nzito dhidi ya uongozi wa juu wa chama hicho, akidai kuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa (bila kumtaja jina moja kwa moja) amezungukwa na watu wasiokuwa na uwezo wa kisiasa wala kiuongozi.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Jingu amesema baadhi ya watu waliomzunguka Mwenyekiti huyo wamekuwa wakitoa ushauri usio na tija, na kwamba ushauri huo umekuwa na athari kubwa kwa mustakabali wa chama, ikiwemo maamuzi ya kufukuza wanachama muhimu.
"Wanampelekea ushauri kama yaliyotokea kwenye uchaguzi, wanamwambia mfukuze fulani, na yeye anakubali. Kwa sababu gani? Kwa sababu hana watu sahihi wa kumshauri katika mambo ya ujenzi wa chama," amesema Jingu.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED