CAG abaina kasoro taa za barabarani Dar

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:08 PM Apr 18 2025
CAG abaina kasoro taa za barabarani Dar
Picha:Mtandao
CAG abaina kasoro taa za barabarani Dar

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), amebaini kuwa ufungaji na matengenezo ya alama za barabarani na taa za kuongoza magari uliofanywa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA), ulikuwa na kasoro.

Katika ukaguzi wa kiufundi wa ufungaji na matengenezo ya vifaa vya barabarani na ishara za mawasiliano ya barabara uliofanywa kwa TANROADS na TARURA umebaini mapungufu katika upangaji wa miradi, usimamizi wa mikataba, na matengenezo, hali ambayo imeathiri kwa kiasi kikubwa usalama wa barabara na ufanisi wa mfumo wa usafirishaji.

Katika Katika Ripoti Kuu ya Mwaka ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2023/24,CAG amebaini kuwa miundombinu ya alama za barabarani katika makutano muhimu jijini Dar es Salaam imepitwa na wakati, hali iliyosababisha hitaji la udhibiti wa foleni kwa mikono kupitia askari wa usalama barabarani.

Aidha, ukosefu wa bajeti ya kutosha umekwamisha juhudi za matengenezo, ambapo Sh. bilioni 1.8 hutengwa kwa mwaka ikilinganishwa na mahitaji halisi ya Sh. bilioni 200.