Wananchi wapanda juu ya mikorosho kupiga simu

By Paul Mabeja , Nipashe
Published at 02:58 PM Apr 15 2025
Mbunge wa Viti Maalum Angelina Malembeka.
Picha: Mtandao
Mbunge wa Viti Maalum Angelina Malembeka.

Mbunge wa viti maalum Angelina Malembeka, amemtaka Waziri wa Mawasiliano na Teknolijia ya Habari Jerry Silaa kwenda Lulindi wilayani Masasi ili kujionea namna wananchi wanavyopata shida kupanda juu ya mikorosho na vichuuguu ili waweze kuwasilina kwa simu kutokana na kukosekana kwa mtandao wa uhakika wa simu.

Amesema hayo leo Aprili 15, bungeni jijini Dodoma wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu katika mwaka wa fedha 2025/2026.

Aidha, amesema kutokana na hali hiyo wananchi wanalazimika kutumia mitandao ya simu kutoka nchi jirani ya Msumbiji.