Wasira: Wanaosubiri CCM kufa, mtasubiri sana

By Maulid Mmbaga , Nipashe
Published at 04:58 PM Apr 15 2025
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Stephan Wasira
Picha: Mpigapicha Wetu
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Stephan Wasira

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Stephan Wasira, amewataka wanachama wa chama hicho kuwa wasiogope kwakuwa hakuna chama kinachowasumbua na wanaosubiri kwamba kitaanguka watasubiri sana.

Akizungumza na wanachama wa CCM Mkoa wa Tabora leo, ambako yuko katika ziara ya kikazi Wasira amesema wanaosubiri CCM itakufa watasubiri sana kwasababu kina mizizi iliyojichimbia chini na inasambaa katika kila nyumba, hivyo viongozi wajisifie chama chao.

'Wanaosubiri CCM kufa, mtasubiri sana'
"CCM ni chama kikubwa Tanzania na Afrika kwa ujumla, wako wanaouliza kwanini hakifi, hawaelewi wala sio siri ni nguvu yetu, kila nyumba kumi kuna kiongozi wa CCM.

"Chama cha namna hiyo huwezi kukiua kwa sababu wenyewe wako kila nyumba 10, wanaobeza chama muwasamehe maana hawajui wanachokifanya, CCM nichama kikubwa Tanazania na Afrika kwa ujumla," amesema Wasira.

'Wanaosubiri CCM kufa, mtasubiri sana'
Ameongeza kuwa chama hicho kina msingi wa watu na kinaanzia kila nyumba 10, akisema wengine wamekuja kujifunza kwao na kwamba hiyo ndio maana ya nguvu yao.