"Watanzania ombeeni Uchaguzi Mkuu, wagombea katafuteni haki ya Mungu"

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:56 PM Apr 15 2025
Mbunge wa Mbogwe (CCM), Nicodemas Maganga.

Mbunge wa Mbogwe (CCM), Nicodemas Maganga, amewaomba watanzania na viongozi wa dini kuombea uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huu huku akiwaasa wenzake wasiwe wanyonge wakatafute haki ya Mungu.Akichangia leo makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2025/26 bungeni , Maganga amesema wabunge waombe Mungu katika faulo watakazocheza na kama kuna kiongozi sio mwaminifu wapigakura wamalizane naye huko huko.