Makalla: Rais Samia amemuelekeza Waziri Mkuu kufika Somanga

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 05:37 PM Apr 15 2025
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla.

Rais Samia Suluhu Hassan amemtaka Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufika katika daraja la Somanga Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi kesho ili kuhakikisha mawasiliano yanarejea katika barabara ya kutoka Dar es salaam kuelekea mikoa ya Kusini.