Yanga watinga nusu fainali kwa kishindo

By Vitus Audax , Nipashe
Published at 06:29 PM Apr 15 2025
Yanga watinga nusu fainali kwa kishindo.
Picha: Yanga
Yanga watinga nusu fainali kwa kishindo.

Timu ya Yanga SC imetinga nusu fainali kombe la CRDB Federation Cup kwa kuifunga Stand United bao 7-1 wakiwafuata Simba SC ambayo ilifuzu kutinga nusu fainali kwa kuichapa Mbeya City bao 3-1.

Yanga SC wanatinga nusu fainali kwa kishindo kutokana na kuifunga Stand United ya Shinyanga bao nyingi zaidi huku wakitarajiwa kukutana na JKT Tanzania katika mchezo wao wa nusu fainali huku Simba SC wakikutana na Singida Black Stars.

Endapo Simba na Yanga watafunzo nusu fainali wanatarajia kukutana fainali katika kombe hilo. Swali linabaki je darby hiyo itachezwa au itasusiwa kama ile ya ligi kuu.

Magoli ya Yanga SC katika mchezo wa leo yamefungwa na Clatous Chama 2 Dk32,41, Stephane Aziz Ki 4 Dk.16, 51, 60, 64, Nickson Kibabage Moja Dk.20 na Kennedy Musonda Moja Dk.86 huku goli pekee la Stand United likifungwa na Msenda Senda Dk.69.