Makalla: CCM kitaendelea kuwa mwalimu wa upinzani

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 05:24 PM May 18 2025
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo  CCM, CPA Amos Makalla
PICHA: MTANDAO
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM, CPA Amos Makalla

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitaendelea kuwa mwalimu wa vyama vingine ili waendelee kujifunza kwao.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo  CCM, CPA Amos Makalla, ametoa kauli hiyo leo Mei 18, 2025, wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Bukoba Mjini, mkoani Kagera, katika ziara yake ya siku saba aliyoianza ikihusisha pia, mikoa mingine ya Geita, Mwanza na Simiyu

"Nilisikia mtani wangu (John) Heche, Makamu Mwenyekiti  CHADEMA amesimama hapa alivyopita na Shinyanga na kwingine kuwaadaa Watanzania wakishika nchi watamlipa kila Mtanzania pensheni.

"Nikajiuliza maswali mawili, huyu mtani wangu amechanganyikiwa, wewe si umesema huendi kwenye uchaguzi, utashikaje nchi, nahisi anaota.

"CCM ndo chama cha siasa kwamba, tunanadi Ilani yetu kuwa tukikamata dola  tutafanya moja, mbili tatu,” amesema Makalla.

Amemuuliza Heche kwamba atalipaje watu pensheni wakati hauko katika watu au chama litakachosimamisha Madiwani, Wabunge na Rais,Uchaguzi Mkuu ujao.