Makalla:CHADEMA msitamani mambo makubwa, madogo yamewashinda

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 05:08 PM May 18 2025
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo  CCM, CPA Amos Makalla
PICHA: MTANDAO
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM, CPA Amos Makalla

KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM, CPA Amos Makalla,amewataka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wasitamani mambo makubwa wakati madogo yamewashinda.

Amedai wanadaiwa na makatibu wa kanda wanane ambao wamesimamishwa kazi, watawezaje kulipa pensheni kwa Watanzania.

Makalla, ameyasema hayo leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Bukoba Mjini, mkoani Kagera, katika ziara yake ya siku saba aliyoianza ikihusisha pia, mikoa mingine ya Geita, Mwanza na Simiyu

"Wanawadai mamilioni ya fedha, utakipa pensheni wakati katibu tu umeshindwa kumlipa," amedai.

Makalla amesema kuna maajabu saba na hilo nalo ni mojawapo ambapo amelileta Makamu Mwenyekiti CHADEMA, John Heche.

"Kwamba, bodaboda atalipwa pensheni, makatibu wa kanda wanane tu wanakushinda wewe ulipe pensheni, mwaka huu tutasikia vituko vingi, huo ni utapeli wa kisiasa," amesema.