Majaliwa: Tutahakikisha kunakuwa na hali ya usalama, uwazi Uchaguzi Mkuu 2025

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:20 PM Apr 15 2025
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali itahakikisha kunakuwa na hali ya usalama, amani, utulivu, uwazi na haki wakati wote wa Uchaguzi Mkuu 2025.

Akihitimiza hoja ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake kwa Mwaka 2025/26, leo Aprili 15,2025, Majaliwa amesema Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imeshakamilisha uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura awamu ya kwanza kwenye mikoa yote na awamu ya pili itaanza Mei, mwaka huu.

Amesema katika maandalizi ya uchaguzi pia daftari hilo litawekwa wazi ili kuwawezesha wapigakura kukagua taarifa zao kwenye kuta za matangazo.

“Nitoe rai kwa watanzania waliopitiwa zoezi la kwanza kutumia fursa hiyo kwenda kujiandikisha na kuboresha taarifa zao awamu ya pili pindi tume itakapotangaza na walioandikishwa wafike kwenye vituo kuhakiki majina yao yatakuwa wazi,”amesema.