JESHI la Polisi mkoani Manyara, limesema watu wawili wanaosadikika kuwa wachimbaji wadogo maarufu wanaapolo ndio wanahofiwa kupotea katika machimbo ya madini ya Tanzanite, Mirerani.
Akizungumza na Nipashe Digital, kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi mkoani Manyara, Ahmed Makarani, amethibitisha huku akisema kutokana na kuwapo kwa taarifa nyingi ambazo hazina uhakika ameelekeza wasaidizi wake kufungua jalada la uchunguzi ili kupata ukweli wa jambo.
"Ni kweli tumefungua jalada la uchunguzi kufatilia hilo jambo, ili tuweze kupata vyanzo sahihi maana imekuwa na vyanzo vingi vipo vinavyosema wamepotea watu nane na vingine vinasema watu tisa," amesema Makarani
Makarani amesema baada ya siku mbili watakuwa kwenye nafasi nzuri ya kujua ukweli ni upi kwa kuwa watakuwa wamepata wazazi ambao wamepotelewa na watoto wao na kuzungumza nao.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED