Mwananfunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Maposeni amefariki dunia huku wengine 64 wakijeruhiwa katika ajali ya trekta walilokuwa wamepanda kukata tela na kupinduka.
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Kapenjama Ndile akizungumza na Nipashe Digital, amesema tukio hilo limetokea Aprili 9,2025 majira ya saa 2 asubuhi katika Kijiji cha Maposeni, Kata ya Peramiho.
Akielezea tukio hilo, Ndile ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Songea, amesema trekta lisilofahamika namba zake za usajili mali ya Mwalimu wa Shule ya Sekondari Maposeni aitwaye Matenga.
Alisema Trekta hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva ambaye hajafahamika jina na kwamba lilitoka shuleni humo kuelekea Kitongoji cha Likwambi jirani na Kijiji cha Lundusi lilikuwa limebeba wanafunzi kidato cha sita.
“Tela lilikatika likapinduka kisha kuacha barabara na kusababisha mwanafunzi mmoja FradyHongo (19) mkazi wa Kijiji cha Lumuli Mafinga mkoani Iringa,”amesema.
Aliwataja majeruhi 11 ni mbaya kuwa ni Edom Mwakisu, Thomas Mwakalemela, Samwel Sheyo, Kasto Burda, Eddi Ibrahimu, Omary Mikidadi, Machimi Bahati, Ambonisye Chritian na Emanuel Mwailonda na kwamba majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali ya Misheni ya Peramiho, na kwamba wengine walitibiwa na kuruhusiwa.
Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi linawashikilia walimu wa Shule ya Sekondari Maposeni amba oni Stephano Kayombo (39) na Geofrey Luambano (48), huku Tedy Nchimbi akishikiliwa kwa kosa la kutosha kielelezo ambacho ni trekta lilokuwa limebeba wanafunzi na dereva ambaye amekimbia.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED