Katika hafla ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Ubungo, Mkuu wa Wilaya hiyo,Albert Msando, ameupokea Mwenge huo na kuwapongeza vijana wanaoukimbiza kwa uzalendo wao pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kinondoni kwa ushirikiano wao katika shughuli hiyo muhimu ya kitaifa.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa Mradi wa Barabara ya Kibwegere–Mpiji Magohe, Msando alieleza kuwa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 1.4 imejengwa kwa gharama ya Shilingi bilioni 2.8 (TZS 2,764,260,330.14) na ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuboresha miundombinu ya barabara katika jiji la Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Saad Mtambule, aliyekabidhi Mwenge huo kwa Wilaya ya Ubungo, alisema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa zaidi ya Shilingi trilioni nne kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Wilaya ya Kinondoni, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.
Msando alitaja miradi saba inayotembelewa na Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Ubungo, yenye jumla ya thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 8.2, kama ifuatavyo:
Miradi hiyo ni sehemu ya juhudi kubwa za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha huduma za kijamii, miundombinu na kuinua ustawi wa wananchi. Kupitia Mwenge wa Uhuru, wananchi wameweza kushuhudia maendeleo yanayoonekana na yanayogusa maisha yao ya kila siku.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED