Heche, Mnyika wapiga mikutano nane Morogoro

By Restuta James , Nipashe
Published at 06:39 PM Jun 06 2025

Viongoizi waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wamefanya mikutano minane ya ‘no reforms, no election’, mkoani Morogoro, wakikumbuka maneno ya hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Picha:Mtandao

Msafara wa Makama Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, umeanzia Mwaya (Kilombero), Ruaha na Mikumi Mjini (Mikumi); wakati wa Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, umeanzia wilayani Kilosa (Dumila, Mvumi na Kimamba); na wote wamehitimisha mikutano hiyo katika mkutano wa hadhara Morogoro Mjini.

Kwenye mikutano yake, Heche, amesema Mwalimu Nyerere, aliwahi kuainisha mambo manne yanayowezesha maendeleo ya nchi, ambayo ni watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.

Amesema Tanzania ina watu wenye utaalamu mbalimbali na ardhi kubwa yenye madini ya kila aina, misitu, rutuba, mito na maziwa, na kwamba kinachokosekana na siasa safi na uongozi bora.

Amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeeneza siasa za propanganda ambazo zimetengeneza ulaghai wakati wa uchaguzi, ikiwamo kutengeneza mazingira ya kuengua wagombea wa vyama vya upinzani, kugombea nafasi za uongozi.

Heche ametoa mfano kwamba katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji mwaka jana, wagombea wengi wa upinzani walienguliwa kwa madai ya kutokujua kusoma na kuandika, ambayo hayakuwa ya kweli.

“Nchi hii kuna siasa chafu, za rushwa, za mauaji, mnachagua watu wanakataliwa. Ndio maana tumesema hatuwezi kwenda kwenye uchaguzi katika mazingira haya,” alisema.

Heche amesema Katiba inataka serikali ifanyekazi kwa lengo la ustawi wa wananchi, ikiwajibika kwa wananchi kwa kujipatia mamlaka kutoka kwa wananchi.

Mnyika, ametoa elimu ya Katiba na sheria za uchaguzi mkoani Morogoro, kwenye mikutano yake ya ‘no reforms, no election.’

Amesema kwenye uchaguzi wa mwaka jana, baadhi ya wagombea wa vijiji wa CHADEMA waliuawa; na kusema hali inaweza kuwa mbaya kwenye uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Amesema engua engua na figisu zilizoonekana kwenye uchaguzi wa vijiji, vitongoji na mitaa, ni dalili mbaya ya uchaguzi wa udiwani, ubunge na urais.