CHAUMMA yapokea wanachama wapya zaidi ya 100 Simiyu

By Elizabeth Zaya , Nipashe
Published at 02:31 PM Jun 06 2025
CHAUMMA yapokea wanachama  wapya zaidi ya 100 Simiyu
Picha:Mpigapicha Wetu
CHAUMMA yapokea wanachama wapya zaidi ya 100 Simiyu

Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimepokea wanachama wapya zaidi ya 100 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Bariadi, mkoani Simiyu.

Wanachama hao wamejiunga rasmi na chama hicho mbele ya umati wa wananchi, ikiwa ni ishara ya kuimarika kwa ushawishi wa CHAUMMA katika eneo hilo.

Kadi za uanachama kwa wanachama hao wapya ziligawiwa na Kaimu Makamu Mwenyekiti wa CHAUMMA Bara, Devotha Minja, ambaye aliwataka wanachama hao kuwa mabalozi wazuri wa chama chao na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kisiasa na maendeleo ya jamii.