Dk. Kimei aonya wanaojipitisha jimboni kwake

By Paul Mabeja , Nipashe
Published at 05:33 PM Apr 11 2025
Mbunge wa Vunjo Dk.Charles Kimei.
Picha: Mtandao
Mbunge wa Vunjo Dk.Charles Kimei.

Mbunge wa Vunjo Dk.Charles Kimei, amewaonya vijana ambao wameanza kujipitisa na kuonesha nia ya kutaka kugombea jimbo hilo katika uchaguzi mkuu 2025.

Dk.Kimei ametoa onyo hilo leo Aprili 11, bungeni jijini Dodoma, wakati akichanagia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu katika mwaka wa Fedha 2025/2026.

“Nataka niwaonye wale vijana wanao jipitishapitisha sasa hivi kule wasije wakaingia kwenye lile daftari la hukumu la CCM la halafu wakashindwa kugombea kwahiyo watulizane na mimi najua wataona kile ambacho tumefanya nini,”amesema Dk. Kimei