Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umepokea tuzo kutoka kwa Makamu wa Rais,Dk. Philip Mpango, ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa Mfuko huo katika kufanikisha Mkutano Mkuu wa 12 wa Chama cha Waandishi Waendesha Ofisi (TAPSEA), unaoendelea Ngurdoto jijini Arusha.
Akizunhumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Meneja Utawala PSSSF Fatma Chondo alisema ni jambo la furaha kwa Mfuko kupata tuzo hiyo na kuahidi kwamba PSSSF itaendelea kufanya kazi kwa karibu na wadau wote ili kuhakikisha kunakuwepo na maendeleo endelevu katika sekta ya hifadhi ya jamii.
Aidha, Katika Mkutano huo PSSSF imeendelea na zoezi la kuchukua alama za vidole kwa wanachama wake wanaoshiriki mkutano huo.
Zoezi hilo linaendeshwa nchi nzima ambapo watumishi wa PSSSF wanapita kwenye maeneo ya kazi na kufanya kazi hiyo kwa lengo la kuboresha taarifa na kurahisisha huduma kwa Wanachama.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED