Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeendelea kuimarisha usimamizi wa sekta ya usafiri wa anga kwa kutekeleza miradi mbalimbali, ikiwemo mradi wa kuboresha mfumo wa mawasiliano ya sauti baina ya mwongoza ndege na rubani.
Prof. Mbarawa ameeleza hayo leo, Alhamisi Mei 15, 2025, bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Katika maelezo yake, Waziri Mbarawa amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo umehusisha kukamilika kwa ufungaji wa mitambo ya mawasiliano ya sauti katika Kituo Mbadala cha Mawasiliano kwa Dharura.
"Sehemu nyimgine ni pamoja na katika viwanja vya ndege vya Julius Nyerere International Airport (JNIA), Abeid Amani Karume International Airport (AAKIA), Kilimanjaro (KIA), Pemba, Tanga, Dodoma, Arusha, Tabora, Kigoma, Mtwara, Mwanza na Songwe," amesema.
Pia Waziri Mbarawa amesisitiza kuwa hatua hizo ni sehemu ya juhudi za serikali kuhakikisha mawasiliano ya haraka, salama na ya uhakika kati ya marubani na waongozaji ndege, hususan katika mazingira ya dharura, ili kuimarisha usalama wa anga nchini.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED