Naibu Katibu Mkuu Bara CHADEMA, Amani Golugwa, amekamatwa na Jeshi la Polisi usiku wa kuamkia leo akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam.
Golugwa alikuwa safarini kuelekea Ubelgiji kukiwakilisha chama katika mkutano wa kimataifa wa International Democracy Union (IDU) unaotarajiwa kuanza rasmi kesho, Mei 14, 2025.
Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na viongozi wa chama hicho, Golugwa alikamatwa ghafla na askari wa Jeshi la Polisi kabla ya kuingia kwenye ndege ya Shirika la Turkish Airlines. Uongozi wa shirika hilo la ndege umeeleza kuwa hajafanikiwa kusafiri.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa kiongozi huyo amepigwa vibaya wakati wa kukamatwa na hadi sasa hajulikani alipo. Simu zake zote hazipatikani, hali inayozua wasiwasi juu ya usalama wake na hali yake.
Taarifa zaidi tutawajuza hapa hapa...
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED