Malasusa: Viongozi wengi tuliobaki tunafeli hapa

By Godfrey Mushi , Nipashe
Published at 12:19 PM May 13 2025

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Alex Malasusa.
Picha: Godfrey Mushi
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Alex Malasusa.

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Alex Malasusa, amesema Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu mstaafu, Hayati, Cleopa Msuya, ushuhuda wake kutoka kwa wananchi wa chini unashangaza.

Malasusa, amesema viongozi wengi wa sasa wanafeli katika kuacha alama, kwa kuwa kwa kifo cha Msuya, kila unayemsikiliza anasifu kwa kile alichokifanya kwenye jamii.

Akihubiri katika ibada maalum ya maziko ya Cleopa Msuya yanayofanyika Usharika wa Usangi Kivindu wa Dayosisi ya Mwanga, Kilimanjaro, Askofu Dk. Malasusa amesema:


"Baba huyu aliyelala, alikuwa ni baba aliyetafuta kuwa na amani wakati wote.Katika viongozi wa serikali waliokuwa serious ni huyu mzee.


"Si kwa sababu alikuwa na nguvu, si kwa sababu ya busara yake, hekima yake. Ushuhuda wa mzee Msuya unanishangaza sana.
...Nimesikia wengi wa ngazi yake waki sifu, hawa wa ngazi za chini wa kisifu. Viongozi wengi tuliobaki tunafeli hapa."


Msuya alifariki dunia Mei 7, 2025 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu.