Mtoto wa kiume wa Hayati Cleopa Msuya, aitwaye Job Msuya, amesema baba yake aliagiza akiondoka duniani, kijengwe Chuo Kikuu cha Mwanga, ambacho hakitumii vitabu vingi kama kumbukizi yake.
Msuya (94) aliyewahi Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu mstaafu, alifariki dunia Mei 7, 2025 katika Hospitali ya Mzena, Jijini Dar es Salaam.
Job amezungumza hayo leo, Mei 13, 2025 katika ibada maalum ya maziko ya baba yake, iliyofanyika Usharika wa Usangi Kivindu wa Dayosisi ya Mwanga ya Kanisa la Kiinjili la Kolutheri Tanzania (KKKT).
"Baba yetu hakupenda kufanyiwa sikukuu yake ya kuzaliwa, lakini mwaka huu; aliagiza afanyiwe na katika sikukuu hiyo, ambayo ilikuwa ni Januari 4 mwaka huu.
"Siku hiyo kulikuwa na mazungumzo mengi kwa wana Mwanga, waliouliza wafanye nini kumuenzi. Wako waliosema apewa jina la Barabara ya By Pass iliyopo Mwanga.
Baadae nilimfuata baba na kumuuliza apewe nini, akanijibu kuwa yeye lengo lake ni kujengewa chuo kikuu katika Wilaya ya Mwanga.
"Nikamuuliza, Chuo Kikuu cha aina gani? akasema sio vile vyuo ambavyo vinatumia vitabu vingi, bali kitakachotumia ubongo cha Technology na Power Brain. ..Pia alisisitiza tuhakikishe Benki ya Wananchi wa Mwanga, Benki aliyoianzisha haifi na tuitunze ili ijekuwa kubwa kama benki nyingine zilizopo nchini."
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED