Mwenyekiti ACT Shinyanga Mjini achukua fomu ya kugombea ubunge

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:29 PM May 12 2025
Mwenyekiti ACT Shinyanga Mjini achukua fomu ya kugombea ubunge.
Picha: Mpigapicha Wetu
Mwenyekiti ACT Shinyanga Mjini achukua fomu ya kugombea ubunge.

Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Jimbo la Shinyanga Mjini, Mbarouk Mohammed Haji, leo amechukua fomu ya kugombea ubunge wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu ujao.

Fomu hiyo imetolewa na Katibu wa ACT Wazalendo wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Juster Denis, katika tukio lililofanyika mbele ya wanachama na wafuasi wa chama hicho.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Mbarouk amesema kuwa ameamua kuwania nafasi hiyo ili kuleta uongozi wa uwajibikaji, ushirikishwaji na maendeleo endelevu kwa wakazi wa Shinyanga Mjini. Alisisitiza kuwa ACT Wazalendo iko tayari kuleta ushindani wa kweli wa kisera kwa ajili ya manufaa ya wananchi.

"Tumejipanga kushindana na CCM kwa hoja na kwa nguvu ya wananchi. Tunaamini kabisa kuwa ushindi unawezekana, na tutaipigania Shinyanga Mjini ili iwe mikononi mwa wananchi," amesema Mbarouk.


Amemalizia kwa kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki mchakato wa uchaguzi na kuwa sehemu ya mabadiliko.