Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda amesema kwa mwaka 2025/26, serikali itaanza utekelezaji na uendeshaji wa Bodi ya Kitaalamu ya Walimu ambayo itawezesha usajili na uendelezaji wa walimu wote walioajiriwa katika shule za serikali na zisizo za serikali.
Akiwasilisha leo bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka 2025/26, Prof. Mkenda amesema “Ili kuhakikisha walimu wanaohitimu katika vyuo vinavyotoa mafunzo ya elimu ya ualimu vinavyotambulika na Serikali wanapata usajili utakaowawezesha kutambulika ndani na nje ya nchi pamoja na kuendeleza utaalamu wao.
Aidha, amesema bodi itawezesha usajili na uendelezaji wa walimu wote walioajiriwa katika shule za serikali na zisizo za Serikali.”
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED