Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewasilisha bungeni bajeti ya Sh.trilioni 2.43 huku ikitangaza kuanza utekelezaji wa mfuko wa “SAMIA Innovation Fund” wenye thamani ya Sh. bilioni 2.3.
Fedha hizo ni kwa ajili ya kutoa mikopo nafuu kwa wabunifu kwa lengo la kuendeleza na kubiasharisha ubunifu pamoja na kutoa fursa za ajira kwa watanzania kupitia kazi za ubunifu.
Alisema katika kutekeleza nia ya kuongeza wataalamu wabobezi katika nyanja ya sayansi na teknolojia ya nyuklia, serikali kupitia SAMIA Extended Skolashipu itaendelea kutoa ufadhili kwa watanzania wenye ufaulu wa juu katika fani za sayansi na teknolojia ya nyuklia kwa ngazi ya shahada ya kwanza ili kuweza kujiunga na masomo ya shahada za juu.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED