WWF inavyopambana na afua ulinzi rasilimali za maji

By Godfrey Mushi , Nipashe
Published at 04:34 PM May 28 2025
Meneja Mradi wa WWF-Tanzania, Novaty Kessy.

Shirika la World Wide Fund for Nature (WWF), limewakutanisha wadau wa sekta ya maji mkoani Kilimanjaro, kujadili, kuongeza nguvu ya mshikamano na utaalam wa kiufundi ulioimarishwa wa afua za ulinzi wa rasilimali za vyanzo vya maji.

Pamoja na mambo mengine, wadau hao wataandaa mpango shirikishi wa ushirikiano, kati ya Mradi wa BMZ-Unganisha Afua za Ulinzi wa Vyanzo vya Maji na Mipango ya Uhifadhi wa Maeneo ya Maji ya Wizara ya Maji (CCPs).

Akizungumza leo, Mei 28, 2025 katika Mji wa Moshi, Meneja Mradi wa WWF-Tanzania, Novaty Kessy, amesema washiriki wanatarajiwa kupata matokeo chanya na yenye tija, ambayo ni pamoja na uelewa wa kitaalamu ulioimarishwa wa afua za ulinzi wa vyanzo vya maji na mafanikio, changamoto na mafunzo.

Wadau hao wanakutana katika warsha ya siku tatu ya kiufundi (TWG), inayolenga zaidi kuoanisha juhudi za uhifadhi wa maeneo yaliyoko chini ya Programu ya SOKNOT Southern Kenya, Northern Tanzania) ulioko chini ya Shirika la World Wildlife Fund (WWF).

 "Bonde la maji linalosimamiwa vizuri na kulindwa linatoa maji yanayotumika katika jamii ikiwa ni pamoja na majisafi ya kunywa, pamoja na kusaidia maisha kama vile kilimo cha umwagiliaji.


"Washiriki wanatarajiwa kupata matokeo chanya na yenye tija kutoka kwenye warsha hii, ambayo ni pamoja na uelewa wa kitaalamu ulioimarishwa wa afua za ulinzi wa vyanzo vya maji, mafanikio, changamoto na mafunzo.