Samia: Ilani mpya ya CCM 2025–2030 kuzinduliwa kesho

By Elizabeth Zaya , Nipashe
Published at 12:06 PM May 29 2025
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Samia Suluhu Hassan.
Picha: Ibrahim Joseph
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Samia Suluhu Hassan.

Mwenyekiti wa CCM Taifa, Samia Suluhu Hassan amesema kesho Mei 30,2025 Ilani ya CCM 2025-2030 itazinduliwa na kwamba imeandaliwa kwa weledi na kushirikisha wadau wote na makundi yote.

Aidha,amesema Ilani hiyo imeanisha vipaumbele vya chama kwa miaka mitano ijayo.

Amesema Ilani iliyopita iliakisi kipindi cha kwanza na ya sasa itaakisi kipindi cha pili na cha mwisho cha 2020-20230.


'Leo tutafanya mapitio ya Ilani ya 2020-2030,matarajio yangu baada ya kupokea utekelezaji wa serikali na kupokea Ilani mpya tutabeba jukumu la kuyatangaza mafanikio ya CCM kwa wananchi,"amesema.


Amesema jana Mei 28,2025 aliweka jiwe la Msingi la aofisi za Makao Mkuu ya CCM itakayojengwa katika Mtaa wa Salimin la ghorofa tano lenye mifumo na tekonolojia ya kisasa na litakamilika 2027 ambapo litazinduliwa wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya CCM.

"Kwa wanachama na wapenzi kuendelea kuunga mkono na kuchangia ujenzi wa ofisi za chama kama ambavyo wamekuwa wakifanya kwenye miradi mingine,"amesema Samia.


Awali,Katibu Mkuu wa CC,Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi amesema malengo ya mkutano huo ni kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025, kuzindua Ilani ya CCM mwaka 2025-2030, na kufanya marekebisho madogo ya katiba ya CCM.

Amesema wajumbe wa mkutano huo ni 1934 wajumbe halali walio 1907 waliofika asilimia 98.6 wajumbe 27 wameomba udhuru na kwa mujibu wa katiba ya CCM akidi ni nusu ya wajumbe,na kwmaba waliopo ni zaidi ya nusu hivyo mkutano huo ni halali.

Vyama rafiki ni kutoka nchi za Afrika Kusini,Msumbiji,Angola,Burundi, China Namibia, Zimbabwe,Uganda,Rwanda,Cuba,Ethiopia,Urusi,Zambia na Korea kusini pia Diaspora kutoka nchi sita.