KESHO ni usiku wa kumpata mbabe wa ligi ya mabingwa barani ulaya kati ya timu ya PSG dhidi ya intermilan.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kutokana na rekodi ya kila timu na namna zilivyofika katika hatua hiyo.Hata hivyo, Tanzania haipo nyuma katika kujifunza namna mashindano hayo makubwa ya kisoka yanavyoandaliwa kupitia hilo kampuni ya Heineken Bverage Tanzania imewafadhili wachambuzi watatu wa mpira wa miguu kwenda ujerumani yanakofanyika mashindano hayo kwa ajili ya kujifunza na baadaye kuleta ujuzi huo nchini.
Wachambuzi hao ni Maulid Kitenge, Shaffih Dauda, pamoja na mwanahabari mashuhuri Joseph "DJ Joozy" Ujumbe huo umeondoka jana jioni utarejea Juni 1 baada ya kushuhudia tukio kubwa zaidi la soka.
Meneja masoko wa kampuni hiyo Lilian Pascal, amesisitiza Heineken, inaelewa soka ni zaidi ya mchezo ni mapenzi ya pamoja ambayo yanawaleta pamoja kwa kuwapa wachambuzi wakuu wa Tanzania uzoefu huu usiosahaulika, hatufadhili safari tu tunakuza sauti za mashabiki wa soka wa taifa letu ambao watakuwa na ari ya kujenga kumbukumbu za wapenda soka nchini kote.
Naye mchambuzi aliyepata nafasi ya kwenda Ujerumani kushuhudia mechi hiyo Maulid Kitenge, amesema Kama mtu ambaye amejitolea kuchambua soka, fursa hii ya kushuhudia fainali ya Ligi ya Mabingwa moja kwa moja ni zaidi ya kile alichofikiria. “Ni heshima kubwa kuwakilisha jamii ya soka ya Tanzania na siwezi kusubiri kurudisha maarifa ya moja kwa moja kwa mashabiki wetu” amesema Kitenge
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED