TAKUKURU Mkoa wa Tanga imeboresha mfumo wa huduma za udhibiti taka ngumu katika jiji la Tanga kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Machi, 2025 ikianza na kata za Central, Chumbageni na Ngamiani Kati.
Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga, Mariamu Mayaya amesema kwa upande wa mifumo katika kipindi husika wamefanikiwa katika utekelezaji wa matakwa ya sheria na kanuni za udhibiti taka ngumu nchini kwa kuntumia mfumo wa punguza, tumia tena na rejeleza taka (PTR).
Amesema pamoja na utekelezaji wa sheria ya udhibiti wa taka ngumu, uchambuzi uliofanywa na TAKUKURU umesaidia mikakati na maazimio ya kulipwa kwa madeni ya wazabuni hivyo kufanya kazi ya uzoaji taka kuanza kutekelezwa kwa ufanisi.
"Kwa ujumla zimefanyika chambuzi za mifumo 20 katika sekta za udhibiti taka na Usafi wa mazingira, afya, kilimo na mapato ambapo tumefanikiwa kubaini mapungufu na kuwasilisha ripoti za chambuzi ambazo zinatekelezwa na mengine yanaendelea kutekelezwa kwa ufanisi" amesema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED