Wanafunzi vyuoni waunda Club ya Nishati Safi kukabiliana na athari za nishati chafu

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 09:44 AM Jun 01 2025
Wanafunzi wa Vyuo vya UDSM, Takwimu, Maji na Ardhi wapata picha ya Pamoja na viongozi waliofika kushuhudia uzinduzi wa club ya Interuniversities Clean Cooking Club katika viwanja vya Takwimu
Picha: Mpigapicha Wetu
Wanafunzi wa Vyuo vya UDSM, Takwimu, Maji na Ardhi wapata picha ya Pamoja na viongozi waliofika kushuhudia uzinduzi wa club ya Interuniversities Clean Cooking Club katika viwanja vya Takwimu

Katika juhudi za kuendeleza kampeni za nishati safi nchini, Wanafunzi wa vyuo vine nchini wameungana ili kuwezesha usambazaji wa elimu na taarifa kuhusu nishati safi kwa wanafunzi wa vyuo mbali mbali na wananchi kwa jumla.

Chini ya uongozi wa kampuni ya Taifa Gas Clean Cooking Unit, wanafunzi hao kutoka vyuo vya Dar es Salaam, Takwimu, Maji na Ardhi, wameunda club iitwayo “Interuniversity Clean Cooking”yenye lengo la Kuongeza uelewa baina ya wanavyuo, kuhusu faida za matumizi ya nishati safi ya kupikia, hususan LPG, kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini.

 Aidha club hiyo ya nishati safi kwa wanafunzi pia inalenga Kuwapa wanafunzi elimu ya usalama, matumizi sahihi na matunzo ya mitungi ya LPG, ikiwa ndiyo nishati ambayo inatumiwa sana na wanafunzi wa vyuo. 

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya takwimu hapa Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Elimu katika Wilaya ya Kinondoni Mutundi Nyamohanga, aliyemuwakilisha Mkuu wa Wilaya Saad Mtambule , alipongeza Taifa Gas, kupitia Idara ya nishati safi kwa kuendeleza kampeni ya nishati safi nchini na hasa kwa kulenga wanafunzi wa vyuo. 

“Hii ni hatua kubwa katika kujenga kizazi cha vijana wanaotambua umuhimu wa kutumia nishati safi ya kupikia kwa afya yao, maendeleo ya jamii, na kulinda mazingira yetu, ndiyo maana naipongeza Taifa Gas kwa hatua hii muhimu. Mchango wenu sio tu wa kiuchumi bali pia wa kijamii” alisema Mutundi. 

1


Mutundi alisema kwamba club hii iliyozinduliwa itawezesha pia kukuza mtandao wa mabalozi wa wanafunzi wanaopigania matumizi ya nishati safi katika jamii na taasisi mbalimbali.

Meneja wa kitengo cha Nishati safi (Clean Cooking and LPG Adoption) Taifa GAS Angellah Bhoke, ambaye ndiye mratibu wa club hiyo, alisema kampuni ya Taifa Gas imeendelea kuipa kipao mbele kampeni ya nishati safi nchini, ikiwa ni mwendelzezo wa kampeini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ya kumtua mama mzigo wa kuni kichwani. 

“Kupitia club hii, nina imani kwamba tutaendelea na mafunzo ya usalama wa gesi (LPG safety training) kwa wanafunzi, hasa wanafunzi wanaojiunga na vyuo kwa mara ya kwanza hata kutoka vyuo vingine. Tutawafikia wadau wengine ili waweze kuunga mkono club hii na malengo yake” alisema Bhoke. 

Mwaka jana, Taifa Gas ilizindua duka la kisasa la gesi kwa ajili ya wanafunzi waishio katika eneo la Changanyikeni ili kuwawezesha kupata nishati safi kwa bei nafuu. Kulingana na Bhoke, duka hilo limeendelea kuwasaidia sana wanafunzi katika upatikaji wa gesi.

“Tunafurahi kwamba duka letu la Campus shop la hapa Changanyikeni linaendelea kutimiza malengo yake ya kuwafikia wanafunzi wote waishio Changanyikeni na viunga vyake, kwa bei nafuu. Wakati wananchi wangine wanajaza gesi ya kilo sita kwa shillingi 23,000, wanafunzi wa Changanyikeni wanajaza gesi hiyo hiyo kwa shillingi 20,000” alisema Bhoke

Aliongeza kuwa; "Hatua hiyo imewasaidia wanafunzi wengi kuendeleza kufika katika duka hilo kujaza gesi na kuboresha afya zao. Aidha, Taifa Gas inawapa wanafunzi hao huduma ya kufikishiwa gesi nyumbani kwa wale ambao wanakosa muda, wilayani Kinondoni —hasa kwa kuwekeza katika duka la kisasa kabisa hapa Changanyikeni, linalolenga kuhudumia wanafunzi kwa bei nafuu.