Rufaa waliotumwa na afande yapigwa kalenda

By Renatha Msungu , Nipashe
Published at 07:22 PM Jun 03 2025
Rufaa waliotumwa na afande yapigwa kalenda
Picha:Mtandao
Rufaa waliotumwa na afande yapigwa kalenda

Kesi ya rufaa inayowakabili watuhumiwa wanne waliopatikana na hatia ya kubaka kwa kundi na kumuingilia kinyume na maumbile binti mmoja mkazi wa Yombo Dovya, Dar es Salaam, imeahirishwa hadi Juni 9, 2025.

Washtakiwa hao walihukumiwa kifungo cha maisha pamoja na kulipa faini ya Shilingi milioni moja kila mmoja, hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma mnamo Septemba 30, 2024.

Jaji Amir Mruma wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, aliyeahirisha kesi hiyo, amesema kuwa itaendelea kusikilizwa tena katika tarehe hiyo iliyopangwa.

Watuhumiwa hao walikutwa na hatia ya kumbaka na kumuingilia kinyume na maumbile binti aliyetambulishwa kwa jina la X, mkazi wa Yombo Dovya, tukio ambalo liliibua taharuki na hasira kwa jamii.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni:

  1. Clinton Damas (MT 140105), askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), maarufu kwa jina la Nyundo.
  2. Praygod Mushi (C.1693), askari wa Magereza.
  3. Nickson Jackson, anayefahamika pia kwa jina la Machuche.
  4. Amin Lema, anayejulikana kwa jina la Kindamba.