Afisa Elimu Mkoa wa Singida, Dk. Elipidius Baganda, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Singida na watumishi wenzake wanne wakikabiliwa na mashtaka 13 likiwamo la utakatishaji fedha Sh.milioni 44.623.
Washtakiwa hao walifikisha mahakamani hapo leo Juni 05, 2025 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Singida, Fadhil Luvinga, na kusomewa mashtaka hayo na Mwendesha Mashtaka upande wa Jamhuri, Marshal Mseja.
Mbali na Dk.Baganda, wengine waliofikishwa mahakamani ni Pasco Kichambati ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Mughanga, Afisa Elimu Maalum Manispaa ya Singida, Deonatus Malima, Afisa Fedha Manispaa ya Singida, Jamanne Lazaro na Mwalimu wa Shule ya Sekondari Mughanga, Evance Mulongo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED